basi usikie huko mbinguni, ukaapo, ukasamehe, ukampatilize kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote; wewe umjuaye moyo; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu);
Methali 15:11 - Swahili Revised Union Version Kuzimu na Uharibifu viko wazi mbele za BWANA; Si zaidi basi, mioyo ya wanadamu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikiwa Mwenyezi-Mungu ajua yaliyo Kuzimu na Abadoni, mawazo ya binadamu yatawezaje kujificha mbele yake? Biblia Habari Njema - BHND Ikiwa Mwenyezi-Mungu ajua yaliyo Kuzimu na Abadoni, mawazo ya binadamu yatawezaje kujificha mbele yake? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikiwa Mwenyezi-Mungu ajua yaliyo Kuzimu na Abadoni, mawazo ya binadamu yatawezaje kujificha mbele yake? Neno: Bibilia Takatifu Mauti na Uharibifu viko wazi mbele za Mwenyezi Mungu: je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu! Neno: Maandiko Matakatifu Mauti na Uharibifu viko wazi mbele za bwana: je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu! BIBLIA KISWAHILI Kuzimu na Uharibifu viko wazi mbele za BWANA; Si zaidi basi, mioyo ya wanadamu? |
basi usikie huko mbinguni, ukaapo, ukasamehe, ukampatilize kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote; wewe umjuaye moyo; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu);
Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na fikira Ndiye Mungu aliye mwenye haki.
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuoneshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,
Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.
na aliye hai; nami nilikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kigiriki analo jina lake Apolioni.
Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.