Akamwambia, Kwa sababu nimesema na Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au, ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa shamba langu la mizabibu.
Methali 14:30 - Swahili Revised Union Version Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amani rohoni humpa mtu afya, lakini tamaa huozesha mifupa. Biblia Habari Njema - BHND Amani rohoni humpa mtu afya, lakini tamaa huozesha mifupa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amani rohoni humpa mtu afya, lakini tamaa huozesha mifupa. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu huozesha mifupa. Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu huozesha mifupa. BIBLIA KISWAHILI Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa. |
Akamwambia, Kwa sababu nimesema na Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au, ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa shamba langu la mizabibu.
Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuondoka, Matumaini ya wasio haki hupotea.
Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.
Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?