Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 15:13 - Swahili Revised Union Version

13 Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Moyo wa furaha hungarisha uso, lakini uchungu huvunja moyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Moyo wa furaha hungarisha uso, lakini uchungu huvunja moyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Moyo wa furaha hung'arisha uso, lakini uchungu huvunja moyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.

Tazama sura Nakili




Methali 15:13
10 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana.


Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; Bali neno jema huufurahisha.


Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa.


Siku zote za mtu ateswaye ni mbaya; Bali ukunjufu wa moyo ni karamu ya daima.


Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.


Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake; Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?


Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.


Kwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu; si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu; tulienenda katika dunia, na hasa kwenu ninyi.


hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi.


Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba iletayo wokovu isiyo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo