Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Methali 13:9 - Swahili Revised Union Version Nuru ya mwenye haki yang'aa sana; Bali taa ya mtu mbaya itazimika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwadilifu hungaa kama taa iwakayo vizuri, lakini waovu ni kama taa inayozimika. Biblia Habari Njema - BHND Mwadilifu hungaa kama taa iwakayo vizuri, lakini waovu ni kama taa inayozimika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwadilifu hung'aa kama taa iwakayo vizuri, lakini waovu ni kama taa inayozimika. Neno: Bibilia Takatifu Nuru ya mwenye haki hung’aa sana, bali taa ya mwovu itazimwa. Neno: Maandiko Matakatifu Nuru ya mwenye haki hung’aa sana, bali taa ya mwovu itazimwa. BIBLIA KISWAHILI Nuru ya mwenye haki yang'aa sana; Bali taa ya mtu mbaya itazimika. |
Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimwa? Na msiba wao kuwajia? Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake?
Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani, Nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake;
Nami nitakapokuzimisha, nitazifunika mbingu, na kuzifanya nyota zake kuwa giza; nami nitalifunika jua kwa wingu, wala mwezi hautatoa nuru yake.
Kwa nini basi jina la baba yetu kufutwa katika jamaa zake kwa sababu alikuwa hana mwana wa kiume? Tupe sisi urithi pamoja na ndugu zake baba yetu.
Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.