Methali 13:11 - Swahili Revised Union Version Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mali ya harakaharaka hutoweka, lakini akusanyaye kidogokidogo ataiongeza. Biblia Habari Njema - BHND Mali ya harakaharaka hutoweka, lakini akusanyaye kidogokidogo ataiongeza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mali ya harakaharaka hutoweka, lakini akusanyaye kidogokidogo ataiongeza. Neno: Bibilia Takatifu Fedha isiyo ya halali hupungua, bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka. Neno: Maandiko Matakatifu Fedha isiyo ya halali hupungua, bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka. BIBLIA KISWAHILI Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa. |
Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.
Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
na mali hizo zimepotea kwa bahati mbaya; naye akiwa amezaa mwana, hamna kitu mkononi mwake.
Kama kware akusanyaye makinda asiyoyaangua, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya maisha yake itamtoka, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.