Methali 12:28 - Swahili Revised Union Version Katika njia ya haki kuna uhai; Wala hakuna mauti katika mapito yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uadilifu ni njia ya uhai, lakini uovu huongoza katika mauti. Biblia Habari Njema - BHND Uadilifu ni njia ya uhai, lakini uovu huongoza katika mauti. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uadilifu ni njia ya uhai, lakini uovu huongoza katika mauti. Neno: Bibilia Takatifu Katika njia ya haki kuna uzima; katika mapito hayo kuna maisha ya milele. Neno: Maandiko Matakatifu Katika njia ya haki kuna uzima; katika mapito hayo kuna maisha ya milele. BIBLIA KISWAHILI Katika njia ya haki kuna uhai; Wala hakuna mauti katika mapito yake. |
Nawe waambie watu hawa, BWANA asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti.
tena ikiwa amezifuata sheria zangu, na kuzishika hukumu zangu; mtu huyu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema Bwana MUNGU.
ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.
Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii.
Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.
Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.