Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




3 Yohana 1:11 - Swahili Revised Union Version

11 Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema anatoka kwa Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema atoka kwa Mwenyezi Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.

Tazama sura Nakili




3 Yohana 1:11
22 Marejeleo ya Msalaba  

Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.


Jiepushe na uovu, utende mema, Na kukaa hata milele.


Usiwafuate walio wengi kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;


Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi hana ufahamu.


Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.


Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.


Mniige mimi kama mimi ninavyomwiga Kristo.


Basi, nawasihi mnifuate mimi.


Hivyo mwigeni Mungu, kama watoto wanaopendwa;


Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.


Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.


Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yudea, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi;


Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu,


ili msiwe wavivu, bali mkawe kama hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.


Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.


Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?


Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.


Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.


Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zipimeni hizo roho, kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo