Methali 12:16 - Swahili Revised Union Version Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Udhia wa mpumbavu hujulikana mara, lakini mwerevu huyapuuza matukano. Biblia Habari Njema - BHND Udhia wa mpumbavu hujulikana mara, lakini mwerevu huyapuuza matukano. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Udhia wa mpumbavu hujulikana mara, lakini mwerevu huyapuuza matukano. Neno: Bibilia Takatifu Mpumbavu huonesha kuudhika kwake mara moja, bali mtu wa busara hupuuza matukano. Neno: Maandiko Matakatifu Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja, bali mtu wa busara hupuuza matukano. BIBLIA KISWAHILI Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu. |
Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika.
Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili.
Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;