Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika shimo mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.
Methali 1:16 - Swahili Revised Union Version Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana wao wako mbioni kutenda maovu, haraka zao zote ni za kumwaga damu. Biblia Habari Njema - BHND Maana wao wako mbioni kutenda maovu, haraka zao zote ni za kumwaga damu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana wao wako mbioni kutenda maovu, haraka zao zote ni za kumwaga damu. Neno: Bibilia Takatifu kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu. Neno: Maandiko Matakatifu kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu. BIBLIA KISWAHILI Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu. |
Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika shimo mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.
Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia zao kuu.
Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.)
Sauli akajaribu kumpiga Daudi hadi ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule.