BWANA huwafumbua macho waliopofuka; BWANA huwainua walioinama; BWANA huwapenda wenye haki;
Mathayo 9:30 - Swahili Revised Union Version Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: “Msimwambie mtu yeyote jambo hili.” Biblia Habari Njema - BHND Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: “Msimwambie mtu yeyote jambo hili.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: “Msimwambie mtu yeyote jambo hili.” Neno: Bibilia Takatifu Macho yao yakafunguka. Isa akawaonya vikali, akisema, “Chungeni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili.” Neno: Maandiko Matakatifu Macho yao yakafunguka. Isa akawaonya vikali, akisema, “Angalieni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili.” BIBLIA KISWAHILI Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue. |
BWANA huwafumbua macho waliopofuka; BWANA huwainua walioinama; BWANA huwapenda wenye haki;
kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.
Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu yeyote habari ya maono hayo, hadi Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.
Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila nenda zako, ukajioneshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
Akamkataza asimwambie mtu, ila, Nenda ukajioneshe kwa kuhani; ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao.