Mathayo 5:6 - Swahili Revised Union Version Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa. Biblia Habari Njema - BHND Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa. Neno: Bibilia Takatifu Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa. Neno: Maandiko Matakatifu Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa. BIBLIA KISWAHILI Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. |
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
Heri mtu yule umchaguaye, Na kumkaribisha akae nyuani mwako. Na tushibe wema wa nyumba yako, Patakatifu pa hekalu lako.
Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai.
Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bibi arusi, Nachuma manemane yangu na rihani, Nala sega la asali na asali yangu, Nanywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.
Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.
Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu; mimi, BWANA, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.
Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;
Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika;
mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.
Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka.
Ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa, kwa kuwa mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia.
lakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Katika siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.
Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala joto iliyo yote.