Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 66:11 - Swahili Revised Union Version

11 mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha, nanyi mtashiba kwa riziki zake; mtakunywa shibe yenu na kufurahi, kutokana na wingi wa fahari yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha, nanyi mtashiba kwa riziki zake; mtakunywa shibe yenu na kufurahi, kutokana na wingi wa fahari yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha, nanyi mtashiba kwa riziki zake; mtakunywa shibe yenu na kufurahi, kutokana na wingi wa fahari yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka katika faraja ya matiti yake; mtakunywa sana, na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka katika faraja ya matiti yake; mtakunywa sana, na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukamua, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.

Tazama sura Nakili

Isaya 66:11
9 Marejeleo ya Msalaba  

Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha kutoka mto wa furaha zako.

Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.

Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.

Utanyonya maziwa ya mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa Yakobo.

Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika makabila ya watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.

Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia.

Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA.

Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu.

Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo