Mathayo 25:18 - Swahili Revised Union Version Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini yule aliyekabidhiwa fedha talanta moja akaenda, akachimba shimo ardhini, akaificha fedha ya bwana wake. Biblia Habari Njema - BHND Lakini yule aliyekabidhiwa fedha talanta moja akaenda, akachimba shimo ardhini, akaificha fedha ya bwana wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini yule aliyekabidhiwa fedha talanta moja akaenda, akachimba shimo ardhini, akaificha fedha ya bwana wake. Neno: Bibilia Takatifu Lakini yule mtumishi aliyekuwa amepokea talanta moja, alienda akachimba shimo ardhini na kuificha ile talanta ya bwana wake. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini yule mtumishi aliyekuwa amepokea talanta moja, alikwenda akachimba shimo ardhini na kuificha ile fedha ya bwana wake. BIBLIA KISWAHILI Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. |
Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.
Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka salama katika kitambaa.
Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.