Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.
Mathayo 22:5 - Swahili Revised Union Version Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake, Biblia Habari Njema - BHND Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake, Neno: Bibilia Takatifu “Lakini hawakuzingatia, wakaenda zao: huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake. Neno: Maandiko Matakatifu “Lakini hawakuzingatia, wakaenda zao: huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake. BIBLIA KISWAHILI Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake; |
Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.
Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng'ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.
akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.
Na Paulo alipokuwa akitoa hoja zake kuhusu haki, na kuwa na kiasi, na hukumu itakayokuja, Feliki akaingiwa na hofu na kusema, Sasa nenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita.
Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
sisi je! Tutapataje kupona, tukipuuza wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliomsikia;
Na kwa tamaa yao watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; wao ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala maangamizi yao hayasinzii.