Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 19:14 - Swahili Revised Union Version

14 Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Basi, Loti akawaendea wachumba wa binti zake, akawaambia, “Haraka! Tokeni mahali hapa, maana Mwenyezi-Mungu atauangamiza mji huu.” Lakini wao wakamwona kama mtu mcheshi tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Basi, Loti akawaendea wachumba wa binti zake, akawaambia, “Haraka! Tokeni mahali hapa, maana Mwenyezi-Mungu atauangamiza mji huu.” Lakini wao wakamwona kama mtu mcheshi tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Basi, Loti akawaendea wachumba wa binti zake, akawaambia, “Haraka! Tokeni mahali hapa, maana Mwenyezi-Mungu atauangamiza mji huu.” Lakini wao wakamwona kama mtu mcheshi tu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa hiyo Lutu alitoka ili kuzungumza na wakwe wake waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa Mwenyezi Mungu yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe wake walifikiri kwamba alikuwa akitania.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa hiyo Lutu alitoka ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa bwana yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe zake walifikiri kwamba alikuwa akitania.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 19:14
26 Marejeleo ya Msalaba  

Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, la sivyo utapotelea katika maangamizi ya mji huu.


Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde popote; ujiponye mlimani, usije ukaangamia.


Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lolote, hadi uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari.


Basi matarishi wakapita mji kwa mji kati ya nchi ya Efraimu na Manase, hata kufika Zabuloni; lakini waliwacheka na kuwadhihaki.


lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.


Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; nendeni, kamtumikieni BWANA kama mlivyosema.


na yeye asiyelitia moyoni neno la BWANA akawaacha watumishi wake na wanyama wake mashambani.


Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafla, wala hapati dawa.


Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, BWANA wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.


Ee BWANA, umenihadaa, nami nimehadaika; wewe una nguvu kuliko mimi, ukashinda; nimekuwa kitu cha kuchekesha, mchana kutwa; kila mtu hunidhihaki.


Ikawa Yeremia alipokwisha kuwaambia watu wote maneno yote ya BWANA, Mungu wao, ambayo BWANA, Mungu wao, amemtuma kwao, yaani, maneno hayo yote,


ndipo Azaria, mwana wa Hoshaya, na Yohana mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakanena, wakimwambia Yeremia, Unasema uongo; BWANA, Mungu wetu, hakukutuma useme, Msiende Misri kukaa huko;


Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.


Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, wao hunisema; Je! Mtu huyu si mtu mwenye kupiga mithali?


Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.


Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao chochote, msiangamizwe katika dhambi zao zote.


Ondokeni kati ya mkutano, ili niwaangamize mara moja. Wao wakaanguka kifudifudi.


Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.


akawaambia, Ondokeni; kwa maana msichana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.


hao waliwaambia mitume habari ya mambo hayo.


Alipokuwa katika kumwendea, pepo akambwaga chini, akamtia kifafa. Yesu akamkemea pepo mchafu, akamponya mtoto, akamrudishia babaye.


Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena kuhusu habari hiyo.


Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo