Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 19:13 - Swahili Revised Union Version

13 maana tutapaharibu mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA; naye BWANA ametutuma tupaharibu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 kwa maana kilio kilichomfikia Mwenyezi-Mungu dhidi ya wakazi wa hapa ni kikubwa mno, naye ametutuma tuje kuwaangamiza.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 kwa maana kilio kilichomfikia Mwenyezi-Mungu dhidi ya wakazi wa hapa ni kikubwa mno, naye ametutuma tuje kuwaangamiza.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 kwa maana kilio kilichomfikia Mwenyezi-Mungu dhidi ya wakazi wa hapa ni kikubwa mno, naye ametutuma tuje kuwaangamiza.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 kwa sababu tunapaangamiza mahali hapa. Kilio kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya watu wa hapa ni kikubwa kiasi kwamba ametutuma kupaangamiza.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 kwa sababu tunapaangamiza mahali hapa. Kilio kwa bwana dhidi ya watu wa hapa ni kikubwa kiasi kwamba ametutuma kupaangamiza.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 maana tutapaharibu mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA; naye BWANA ametutuma tupaharibu.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 19:13
21 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya BWANA.


BWANA akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,


Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Wakwe, wanao wa kiume au wa kike, na wowote ulio nao katika mji uwatoe katika mahali hapa;


Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa malipo ya mikono yake.


Je! Nimepanda mimi, ili kupigana na mahali hapa na kupaangamiza, bila shauri la BWANA? BWANA ndiye aliyeniambia, Panda upigane na nchi hii na kuiangamiza.


Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.


Hata BWANA asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.


Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.


Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.


Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.


Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza;


naziita mbingu na nchi hivi leo kushuhudia, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa.


Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliokosa kuwalipa kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.


Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo