Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale;
Mathayo 22:42 - Swahili Revised Union Version Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nyinyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Wa Daudi.” Biblia Habari Njema - BHND “Nyinyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Wa Daudi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nyinyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Wa Daudi.” Neno: Bibilia Takatifu “Mnaonaje kuhusu Al-Masihi? Yeye ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.” Neno: Maandiko Matakatifu “Mnaonaje kuhusu Al-Masihi? Yeye ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Yeye ni Mwana wa Daudi.” BIBLIA KISWAHILI Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. |
Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale;
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi.
Hapo hapana Mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutotahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala muungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.