Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
Mathayo 21:10 - Swahili Revised Union Version Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu, mji wote ukajaa ghasia. Watu wakawa wanauliza, “Huyu ni nani?” Biblia Habari Njema - BHND Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu, mji wote ukajaa ghasia. Watu wakawa wanauliza, “Huyu ni nani?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu, mji wote ukajaa ghasia. Watu wakawa wanauliza, “Huyu ni nani?” Neno: Bibilia Takatifu Isa alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” Neno: Maandiko Matakatifu Isa alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” BIBLIA KISWAHILI Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? |
Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
wakamwambia, wakisema, Tuambie, unatenda mambo hayo kwa mamlaka gani? Tena, ni nani aliyekupa mamlaka haya?
Basi, wale Waandishi na Mafarisayo wakaanza kuulizana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?
Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao, Ni nani huyu hata asamehe dhambi?
Lakini Herode akasema, Yohana nilimkata kichwa; basi ni nani huyu ambaye ninasikia mambo haya juu yake? Akataka kumwona.
Hivyo hao wakaendelea wote wawili hadi walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote uliwaajabia. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi?
Samweli akafanya hayo aliyosema BWANA, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani?