Mathayo 17:7 - Swahili Revised Union Version Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, “Simameni, msiogope!” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, “Simameni, msiogope!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, “Simameni, msiogope!” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Isa akaja na kuwagusa, akawaambia, “Inukeni na wala msiogope.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Isa akaja na kuwagusa, akawaambia, “Inukeni na wala msiogope.” BIBLIA KISWAHILI Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope. |
Basi alipokuwa akisema nami, nilishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.
naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.
nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hadi nchini, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?
Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,