Marko 4:3 - Swahili Revised Union Version Sikilizeni; Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. Biblia Habari Njema - BHND “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. Neno: Bibilia Takatifu “Sikilizeni! Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu Neno: Maandiko Matakatifu “Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. BIBLIA KISWAHILI Sikilizeni; Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda; |
Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiulegeze mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.
Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani;
Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika shamba lake;
Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Yudea, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.
Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.
Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.