Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nilikuwa mume kwao, asema BWANA.
Luka 8:54 - Swahili Revised Union Version Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Yesu akamshika mkono akasema, “Mtoto, amka!” Biblia Habari Njema - BHND Lakini Yesu akamshika mkono akasema, “Mtoto, amka!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Yesu akamshika mkono akasema, “Mtoto, amka!” Neno: Bibilia Takatifu Isa akamshika yule binti mkono na kuita, “Binti, amka!” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamshika yule binti mkono na kuita, “Binti, amka!” BIBLIA KISWAHILI Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka. |
Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nilikuwa mume kwao, asema BWANA.
Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate katika macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
Alipofika nyumbani hakuruhusu mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.
Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao.
Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, inuka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.
(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.