Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande katika mashua na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.
Luka 8:22 - Swahili Revised Union Version Ikawa siku zile mojawapo alipanda katika mashua yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ngambo.” Basi, wakaanza safari. Biblia Habari Njema - BHND Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ngambo.” Basi, wakaanza safari. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ng'ambo.” Basi, wakaanza safari. Neno: Bibilia Takatifu Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa.” Nao wakaondoka. Neno: Maandiko Matakatifu Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni twende mpaka ng’ambo ya ziwa.” Nao wakaondoka. BIBLIA KISWAHILI Ikawa siku zile mojawapo alipanda katika mashua yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga. |
Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande katika mashua na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.
Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika ile mashua, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.
Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani, watangulie kwenda ng'ambo hata Bethsaida, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.
Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,
Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, mashua ikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi liliteremka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji.
Tukapanda katika merikebu ya Adramitio iliyokuwa tayari kusafiri mpaka miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedonia wa Thesalonike, akiwa pamoja nasi.