Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
Luka 22:57 - Swahili Revised Union Version Akakana, akisema, Ee mwanamke, simjui. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Petro akakana akisema, “Wee! Simjui mimi.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini Petro akakana akisema, “Wee! Simjui mimi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Petro akakana akisema, “Wee! Simjui mimi.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Petro akakana, akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Petro akakana, akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” BIBLIA KISWAHILI Akakana, akisema, Ee mwanamke, simjui. |
Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi akiwa katika mwanga, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye.
Muda mfupi baadaye mtu mwingine alimwona akasema, Wewe nawe u mmoja wao. Petro akasema, Ee mtu, si mimi.
Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anakota moto. Basi wakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo? Naye akakana, akasema, Si mimi.
Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.