Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
Luka 18:28 - Swahili Revised Union Version Petro akasema, Tazama, sisi tumeviacha vitu vyetu vyote na kukufuata. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Petro akamwuliza, “Na sisi, je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!” Biblia Habari Njema - BHND Naye Petro akamwuliza, “Na sisi, je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Petro akamwuliza, “Na sisi, je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!” Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwa navyo tukakufuata!” Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwa navyo tukakufuata!” BIBLIA KISWAHILI Petro akasema, Tazama, sisi tumeviacha vitu vyetu vyote na kukufuata. |
Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.
Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.
Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, niliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.