Kwa maana anaweza kutoka gerezani kutawala; hata ikiwa alizaliwa akiwa maskini katika ufalme.
Luka 1:52 - Swahili Revised Union Version Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewainua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu. Biblia Habari Njema - BHND amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu. Neno: Bibilia Takatifu Amewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya utawala, lakini amewainua wanyenyekevu. Neno: Maandiko Matakatifu Amewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya enzi, lakini amewainua wanyenyekevu. BIBLIA KISWAHILI Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewainua. |
Kwa maana anaweza kutoka gerezani kutawala; hata ikiwa alizaliwa akiwa maskini katika ufalme.
Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, BWANA, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.
Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale;
Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na dada zake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.