Luka 1:30 - Swahili Revised Union Version Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. Biblia Habari Njema - BHND Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu; umepata kibali kwa Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu, umepata kibali kwa Mwenyezi Mungu. BIBLIA KISWAHILI Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. |
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema BWANA, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.
BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.
Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.
Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yohana.
akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.