Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Luka 1:30 - Swahili Revised Union Version

30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu; umepata kibali kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu, umepata kibali kwa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.

Tazama sura Nakili




Luka 1:30
13 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.


usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.


Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema BWANA, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.


BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.


Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo, ni mimi; msiogope.


Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.


Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yohana.


Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.


akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.


Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?


Hata tunathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo