Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 44:2 - Swahili Revised Union Version

2 BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Mimi, Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyekufanya tangu tumboni mwa mama yako, nimekuja kukusaidia wewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Usiogope, ewe taifa la Yakobo, mtumishi wangu, naam, usiogope ewe Yeshuruni mteule wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Mimi, Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyekufanya tangu tumboni mwa mama yako, nimekuja kukusaidia wewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Usiogope, ewe taifa la Yakobo, mtumishi wangu, naam, usiogope ewe Yeshuruni mteule wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Mimi, Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyekufanya tangu tumboni mwa mama yako, nimekuja kukusaidia wewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Usiogope, ewe taifa la Yakobo, mtumishi wangu, naam, usiogope ewe Yeshuruni mteule wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni, yeye atakayekusaidia: Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu, Yeshuruni, niliyekuchagua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Hili ndilo asemalo bwana, yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni, yeye atakayekusaidia: Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu, Yeshuruni, niliyekuchagua.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.

Tazama sura Nakili




Isaya 44:2
29 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu yu katikati ya mji hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.


Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.


Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.


Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.


usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.


Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema BWANA, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.


Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Abrahamu, rafiki yangu;


Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.


watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu.


Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi;


Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.


Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi.


BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?


BWANA, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni.


Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi makabila ya watu mlio mbali sana; BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu.


Na sasa BWANA asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya BWANA, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu);


Kabla sijakuumba katika tumbo nilikujua, na kabla hujatoka tumboni, nilikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.


Kwa sababu hiyo usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema BWANA; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.


Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.


Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.


kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.


Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.


Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake.


Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja.


Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, tunajua uteule wenu;


Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo