Isaya 33:9 - Swahili Revised Union Version Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nchi inaomboleza na kunyauka; misitu ya Lebanoni imekauka, bonde zuri la Sharoni limekuwa jangwa, huko Bashani na mlimani Karmeli miti imepukutika majani yake. Biblia Habari Njema - BHND Nchi inaomboleza na kunyauka; misitu ya Lebanoni imekauka, bonde zuri la Sharoni limekuwa jangwa, huko Bashani na mlimani Karmeli miti imepukutika majani yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nchi inaomboleza na kunyauka; misitu ya Lebanoni imekauka, bonde zuri la Sharoni limekuwa jangwa, huko Bashani na mlimani Karmeli miti imepukutika majani yake. Neno: Bibilia Takatifu Ardhi inaomboleza na kuchakaa, Lebanoni imeaibika na kunyauka; Sharoni ni kama Araba, nayo Bashani na Karmeli wanapukutisha majani yao. Neno: Maandiko Matakatifu Ardhi inaomboleza na kuchakaa, Lebanoni imeaibika na kunyauka, Sharoni ni kama Araba, nayo Bashani na Karmeli wanapukutisha majani yao. BIBLIA KISWAHILI Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani. |
naye atavikata vichaka vya msitu kwa chuma; na Lebanoni utaanguka kwa mkono wake aliye mwenye uweza.
Naam, misonobari inakufurahia, Na mierezi ya Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti aliyetujia.
Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani;
Tazama, BWANA ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake.
ndipo nitamwudhi Arieli; kutakuwapo maombolezo na kilio; naye atakuwa kwangu kama Arieli.
Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa BWANA, ukuu wa Mungu wetu.
Umemshutumu Bwana kwa watumishi wako, kwa kuwa umesema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani ya Lebanoni; nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misonobari yake mizuri, nami nitaingia ndani ya mahali pake palipoinuka, palipo mbali sana, msitu wa shamba lake lizaalo sana.
Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng'ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta.
Nami nitamleta Israeli tena malishoni kwake, naye atalisha juu ya Karmeli, na Bashani, na nafsi yake itashiba juu ya milima ya Efraimu, na katika Gileadi.
Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa porini na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataangamizwa.
Naye alisema, BWANA atanguruma toka Sayuni, Atatoa sauti yake toka Yerusalemu; Na malisho ya wachungaji yatakauka, Na kilele cha Karmeli kitanyauka.
Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, msituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.
Yeye huikemea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote; Bashani hulegea, na Karmeli; nalo ua la Lebanoni hulegea.
Tukatwaa miji yake yote wakati huo; hapakuwa na mji tusiotwaa kwao miji sitini, nchi yote ya Argobu, ndio ufalme wa Ogu ulio katika Bashani.