Hosea 5:14 - Swahili Revised Union Version Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, kama mwanasimba kwa watu wa Yuda. Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka, nitawachukua na hakuna atakayewaokoa. Biblia Habari Njema - BHND Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, kama mwanasimba kwa watu wa Yuda. Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka, nitawachukua na hakuna atakayewaokoa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, kama mwanasimba kwa watu wa Yuda. Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka, nitawachukua na hakuna atakayewaokoa. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu, kama simba mkubwa kwa Yuda. Nitawararua vipande vipande na kuondoka; nitawachukua mbali, na hakuna wa kuwaokoa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu, kama simba mkubwa kwa Yuda. Nitawararua vipande vipande na kuondoka; nitawachukua mbali, na hakuna wa kuwaokoa. BIBLIA KISWAHILI Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa. |
Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wanasimba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.
Ameacha mahali pake pa kujificha, kama simba; maana nchi yao imekuwa kitu cha kushangaza, kwa sababu ya ukali wa upanga uoneao, na kwa sababu ya hasira yake kali.
Kwa kadiri ya malisho yao, kwa kadiri iyo hiyo walishiba; walishiba na moyo wao ukatukuka; ndiyo sababu wamenisahau mimi.
Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila.
Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu.
Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio; Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake; Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;
Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwanasimba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyagakanyaga na kuraruararua, wala hakuna wa kuokoa.
Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang'anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo wako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa.
Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,