Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 5:29 - Swahili Revised Union Version

29 Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wanasimba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Askari wao wananguruma kama simba; wananguruma kama wanasimba ambao wamekamata mawindo yao na kuwapeleka mahali mbali ambapo hakuna awezaye kuwanyanganya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Askari wao wananguruma kama simba; wananguruma kama wanasimba ambao wamekamata mawindo yao na kuwapeleka mahali mbali ambapo hakuna awezaye kuwanyanganya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Askari wao wananguruma kama simba; wananguruma kama wanasimba ambao wamekamata mawindo yao na kuwapeleka mahali mbali ambapo hakuna awezaye kuwanyang'anya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Ngurumo yao ni kama ile ya simba, wananguruma kama wana simba, wanakoroma wanapokamata mawindo yao, na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Ngurumo yao ni kama ile ya simba, wananguruma kama wana simba, wanakoroma wanapokamata mawindo yao, na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

29 Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wanasimba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.

Tazama sura Nakili




Isaya 5:29
20 Marejeleo ya Msalaba  

Yuda ni mwanasimba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha?


Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane wa kuwaokoa.


Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.


Maana BWANA aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwanasimba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo BWANA wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake.


Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.


Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.


Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatangatanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.


Wanasimba wamenguruma juu yake, wametoa sana sauti zao; Nao wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; miji yake imeteketea, haina watu.


Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa; ameanza kushika njia, ametoka katika mahali pake; ili aifanye nchi yako kuwa ukiwa, miji yako ifanywe maganjo, asibaki mwenyeji ndani yake.


Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafla ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?


Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadneza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.


Watanguruma pamoja kama wanasimba; watanguruma kama simba wachanga.


Watakwenda kumfuata BWANA, atakayenguruma kama simba; kwa maana atanguruma, nao watoto watakuja kutoka magharibi wakitetemeka.


Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?


Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwanasimba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyagakanyaga na kuraruararua, wala hakuna wa kuokoa.


Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wanasimba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwanasimba, wala hapana aliyewatia hofu?


Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi.


Sikiza, maombolezo ya wachungaji, Kwa maana utukufu wao umeharibiwa; Sikiza, ngurumo za simba, Kwa maana vichaka vya Yordani vimeharibiwa!


Aliinama, akalala mfano wa simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha? Na abarikiwe kila akubarikiye, Na alaaniwe kila akulaaniye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo