Hosea 4:17 - Swahili Revised Union Version Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Watu wa Efraimu wamejifunga na sanamu. Haya! Waache waendelee tu! Biblia Habari Njema - BHND “Watu wa Efraimu wamejifunga na sanamu. Haya! Waache waendelee tu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Watu wa Efraimu wamejifunga na sanamu. Haya! Waache waendelee tu! Neno: Bibilia Takatifu Efraimu amejiunga na sanamu, achana naye! Neno: Maandiko Matakatifu Efraimu amejiunga na sanamu, ondokana naye! BIBLIA KISWAHILI Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache. |
Kadiri walivyowaita ndivyo walivyoondoka na kuwaacha; waliwatolea dhabihu Mabaali, na kuzifukizia uvumba sanamu za kuchonga.
Na upanga utaiangukia miji yake, utayaharibu makomeo yake na kuyala, kwa sababu ya mashauri yao wenyewe.
Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.
Na sasa wanazidi kufanya dhambi, nao wamejifanyia sanamu kwa fedha yao, naam, sanamu kwa kadiri ya akili zao; zote pia ni kazi ya mafundi; nao huzitaja hivi, Wanaume watoao dhabihu na wazibusu ndama.
Lakini asishindane mtu, wala mtu asikemee; maana watu wako ni kama wao washindanao na kuhani.
Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.
Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.