Akasema, Niliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji. BWANA akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.
Hesabu 24:3 - Swahili Revised Union Version Akatunga mithali yake, akasema, Balaamu mwana wa Beori asema, Yule mtu aliyefumbuliwa macho asema; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema naye akatamka kauli hii ya kinabii: Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Peori kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho; Biblia Habari Njema - BHND naye akatamka kauli hii ya kinabii: Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Peori kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza naye akatamka kauli hii ya kinabii: Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Peori kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho; Neno: Bibilia Takatifu naye akatoa ujumbe wake: “Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori, ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri; Neno: Maandiko Matakatifu naye akatoa ujumbe wake: “Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori, ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri; BIBLIA KISWAHILI Akatunga mithali yake, akasema, Balaamu mwana wa Beori asema, Yule mtu aliyefumbuliwa macho asema; |
Akasema, Niliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji. BWANA akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.
Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nilimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kulia na wa kushoto.
Ndipo BWANA akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, akiwa na upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa, naye akainamisha kichwa, akaanguka kifudifudi.
Naye akatunga mithali yake, akasema, Ondoka Balaki, ukasikilize; Nisikilize, Ee mwana wa Sipori;
Akatunga mithali yake, akasema, Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki, Njoo! Unilaanie Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli.
Akatunga mithali yake akasema, Balaamu mwana wa Beori asema, Yule mtu aliyefumbwa macho asema,
Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu. Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho,
Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho;