Amosi 2:3 - Swahili Revised Union Version nami nitamkatilia mbali mwamuzi atoke kati yake, nami nitawaua wakuu wake pamoja naye, asema BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Isitoshe, nitamuua mtawala wa Moabu, pamoja na viongozi wote wa nchi hiyo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” Biblia Habari Njema - BHND Isitoshe, nitamuua mtawala wa Moabu, pamoja na viongozi wote wa nchi hiyo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Isitoshe, nitamuua mtawala wa Moabu, pamoja na viongozi wote wa nchi hiyo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” Neno: Bibilia Takatifu Nitamwangamiza mtawala wake na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,” asema Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Nitamwangamiza mtawala wake na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,” asema bwana. BIBLIA KISWAHILI nami nitamkatilia mbali mwamuzi atoke kati yake, nami nitawaua wakuu wake pamoja naye, asema BWANA. |
Pembe ya Moabu imekatika, na mkono wake umevunjika, asema BWANA. Mlevyeni; kwa maana alijitukuza juu ya BWANA
Maana, kwa kuwa umeyatumainia matendo yako, na hazina zako, wewe nawe utatwaliwa; na Kemoshi atatoka aende katika uhamisho, makuhani wake na wakuu wake pamoja.
Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.
Je! Farasi watapiga mbio juu ya mwamba? Je! Mtu atalima kwa plau na ng'ombe baharini? Hata mmegeuza hukumu kuwa sumu, na matunda ya haki kuwa uchungu;
Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipigapiga pembe za Moabu, Na kuwavunjavunja wana wote wa ghasia.