Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Amosi 2:2 - Swahili Revised Union Version

2 lakini nitatuma moto juu ya Moabu, nao utayateketeza majumba ya Keriothi; na Moabu atakufa pamoja na mshindo, na kelele, na sauti ya tarumbeta;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Basi, nitaishushia moto nchi ya Moabu, na kuziteketeza kabisa ngome za mji wa Keriothi. Wanajeshi watakapopaza sauti zao na kupiga tarumbeta, watu wa Moabu watakufa katika makelele hayo ya vita.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Basi, nitaishushia moto nchi ya Moabu, na kuziteketeza kabisa ngome za mji wa Keriothi. Wanajeshi watakapopaza sauti zao na kupiga tarumbeta, watu wa Moabu watakufa katika makelele hayo ya vita.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Basi, nitaishushia moto nchi ya Moabu, na kuziteketeza kabisa ngome za mji wa Keriothi. Wanajeshi watakapopaza sauti zao na kupiga tarumbeta, watu wa Moabu watakufa katika makelele hayo ya vita.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Nitatuma moto juu ya Moabu ambao utateketeza ngome za Keriothi. Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa katikati ya kelele za vita, na sauti ya tarumbeta.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Nitatuma moto juu ya Moabu ambao utateketeza ngome za Keriothi. Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa katikati ya vilio vya vita na mlio wa tarumbeta.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 lakini nitatuma moto juu ya Moabu, nao utayateketeza majumba ya Keriothi; na Moabu atakufa pamoja na mshindo, na kelele, na sauti ya tarumbeta;

Tazama sura Nakili

Amosi 2:2
8 Marejeleo ya Msalaba  

Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyovingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.

na juu ya Keriothi, na juu ya Bozra, na juu ya miji yote ya nchi ya Moabu, iliyo mbali na iliyo karibu.

Toka kilio cha Heshboni mpaka Eleale, naam, mpaka Yahasa, wametoa sauti zao, toka Soari mpaka Horonaimu, hata Eglath-shelishia; maana maji ya Nimrimu nayo yatakuwa ukiwa.

Miji imetwaliwa, ngome zimeshambuliwa, na mioyo ya mashujaa wa Moabu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.

Wamekimbia, wasio na nguvu Wanasimama chini ya kivuli cha Heshboni; Ila moto umetoka katika Heshboni, Na muali wa moto toka kati ya Sihoni Nao umekula pembe ya Moabu, Na utosi wa kichwa wa watu wapigao kelele.

Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu Moabu na Seiri husema, Tazama, nyumba ya Israeli ni sawasawa na mataifa yote;

lakini nitawasha moto katika ukuta wa Raba, nao utayateketeza majumba yake; pamoja na kupiga kelele siku ya vita, pamoja na tufani katika siku ya chamchela;

lakini nitatuma moto uingie katika nyumba ya Hazaeli, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo