Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Amosi 6:12 - Swahili Revised Union Version

12 Je! Farasi watapiga mbio juu ya mwamba? Je! Mtu atalima kwa plau na ng'ombe baharini? Hata mmegeuza hukumu kuwa sumu, na matunda ya haki kuwa uchungu;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Je, farasi waweza kupiga mbio miambani? Je, watu huilima bahari kwa ng'ombe? Lakini nyinyi mmeigeuza haki kuwa sumu, na tunda la uadilifu kuwa uchungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Je, farasi waweza kupiga mbio miambani? Je, watu huilima bahari kwa ng'ombe? Lakini nyinyi mmeigeuza haki kuwa sumu, na tunda la uadilifu kuwa uchungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Je, farasi waweza kupiga mbio miambani? Je, watu huilima bahari kwa ng'ombe? Lakini nyinyi mmeigeuza haki kuwa sumu, na tunda la uadilifu kuwa uchungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Je, farasi wanaweza kukimbia kwenye miamba iliyochongoka? Je, mtu aweza kulima kwa maksai huko? Lakini mmegeuza haki kuwa sumu na matunda ya uadilifu kuwa uchungu:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Je, farasi waweza kukimbia kwenye miamba mikali? Je, aweza mtu kulima huko kwa maksai? Lakini mmegeuza haki kuwa sumu na matunda ya uadilifu kuwa uchungu:

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Je! Farasi watapiga mbio juu ya mwamba? Je! Mtu atalima kwa plau na ng'ombe baharini? Hata mmegeuza hukumu kuwa sumu, na matunda ya haki kuwa uchungu;

Tazama sura Nakili

Amosi 6:12
17 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa sababu nilijua ya kuwa wewe u mkaidi, na shingo yako ni shingo ya chuma, na kipaji cha uso wako ni shaba;

Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.

Mmelima dhuluma, mmevuna uovu; mmekula matunda ya uongo; kwa maana uliitumainia njia yako, na wingi wa mashujaa wako.

Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba.

nami nitamkatilia mbali mwamuzi atoke kati yake, nami nitawaua wakuu wake pamoja naye, asema BWANA.

Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.

Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini,

Mikono yao ni hodari kwa kutenda maovu; afisa na hakimu wanataka rushwa, mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.

Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo