2 Samueli 22:33 - Swahili Revised Union Version Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara, na ameifanya njia yangu iwe salama. Biblia Habari Njema - BHND Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara, na ameifanya njia yangu iwe salama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara, na ameifanya njia yangu iwe salama. Neno: Bibilia Takatifu Mungu ndiye anivikaye nguvu, na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. Neno: Maandiko Matakatifu Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. BIBLIA KISWAHILI Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake. |
Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?
Nitakuwa na mwenendo usio na hatia; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu.
Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.
BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
Nami nitawatia nguvu katika BWANA; nao watatembea huku na huko katika jina lake, asema BWANA.
Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.