Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 22:33 - Swahili Revised Union Version

33 Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara, na ameifanya njia yangu iwe salama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara, na ameifanya njia yangu iwe salama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara, na ameifanya njia yangu iwe salama.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Mungu ndiye anivikaye nguvu, na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

33 Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake.

Tazama sura Nakili




2 Samueli 22:33
19 Marejeleo ya Msalaba  

akasema, BWANA ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu,


Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?


Nitakuwa na mwenendo usio na hatia; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu.


Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.


Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA.


Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu.


BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?


Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.


Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.


BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.


usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.


Nami nitawatia nguvu katika BWANA; nao watatembea huku na huko katika jina lake, asema BWANA.


Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.


Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.


Uwe mkamilifu kwa BWANA, Mungu wako.


Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.


awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo