BWANA alinitendea kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu akanilipa.
2 Samueli 22:25 - Swahili Revised Union Version Basi BWANA amenilipa kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu mbele zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu amenituza kadiri ya uadilifu wangu, yeye anajua usafi wangu. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu amenituza kadiri ya uadilifu wangu, yeye anajua usafi wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu amenituza kadiri ya uadilifu wangu, yeye anajua usafi wangu. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu amenilipa sawasawa na uadilifu wangu, sawasawa na usafi wangu machoni pake. Neno: Maandiko Matakatifu bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu, sawasawa na usafi wangu machoni pake. BIBLIA KISWAHILI Basi BWANA amenilipa kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu mbele zake. |
BWANA alinitendea kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu akanilipa.
Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.
Ikiwa, mwenye haki atalipwa duniani; Je, mwovu na mkosaji hawatalipwa mara nyingi zaidi?
Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari.
Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee malipo ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, yawe ni mema au mabaya.
BWANA humlipa kila mtu kulingana na haki na uaminifu wake; maana BWANA amekutia mikononi mwangu leo, nami nilikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA.