Basi BWANA amenilipa kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu mbele zake.
2 Samueli 22:21 - Swahili Revised Union Version BWANA alinitendea kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu akanilipa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu; alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia. Biblia Habari Njema - BHND “Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu; alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu; alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia. Neno: Bibilia Takatifu “Mwenyezi Mungu alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. Neno: Maandiko Matakatifu “bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. BIBLIA KISWAHILI BWANA alinitendea kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu akanilipa. |
Basi BWANA amenilipa kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu mbele zake.
Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.
basi, usikie huko mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumwa wako; ukimpatiliza mtu mbaya, kwa kuleta njia yake juu ya kichwa chake; na kumpa mwenye haki haki yake, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake.
Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiweka nafsi yake katika uongo, Wala hakuapa kwa hila.
BWANA atawaamua mataifa, BWANA, unihukumu mimi, Kwa kadiri ya haki yangu, Kulingana na unyofu nilio nao.
Ikiwa, mwenye haki atalipwa duniani; Je, mwovu na mkosaji hawatalipwa mara nyingi zaidi?
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
BWANA humlipa kila mtu kulingana na haki na uaminifu wake; maana BWANA amekutia mikononi mwangu leo, nami nilikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA.