Basi Abneri akafanya mashauri na wazee wa Israeli, akasema, Zamani mlitaka Daudi awamiliki;
1 Samueli 8:4 - Swahili Revised Union Version Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, viongozi wote wa Israeli walikusanyika pamoja, na kumwendea Samueli mjini Rama, Biblia Habari Njema - BHND Basi, viongozi wote wa Israeli walikusanyika pamoja, na kumwendea Samueli mjini Rama, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, viongozi wote wa Israeli walikusanyika pamoja, na kumwendea Samueli mjini Rama, Neno: Bibilia Takatifu Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama. Neno: Maandiko Matakatifu Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama. BIBLIA KISWAHILI Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; |
Basi Abneri akafanya mashauri na wazee wa Israeli, akasema, Zamani mlitaka Daudi awamiliki;
Basi wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni, naye mfalme Daudi akapatana nao huko Hebroni mbele za BWANA; wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya Israeli.
Kisha BWANA akamwambia Musa, Kweeni wewe, na Haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini wa wazee wa Israeli, mkamfikie BWANA; mkasujudie kwa mbali;
Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri;
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaomba mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka.
Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, Tuachie siku saba, ili tutume wajumbe waende kote mipakani mwa Israeli; kisha, ikiwa hakuna atakayetuokoa, tutajisalimisha kwako.
Kisha alikuwa akirudi Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Waisraeli; na huko akamjengea BWANA madhabahu.