Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 3:16 - Swahili Revised Union Version

16 Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli na kuwaambia: Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu: Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea na kusema, ‘Nimewachunguzeni na kuyaona mambo mnayotendewa nchini Misri!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli na kuwaambia: Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu: Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea na kusema, ‘Nimewachunguzeni na kuyaona mambo mnayotendewa nchini Misri!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli na kuwaambia: Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu: Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea na kusema, ‘Nimewachunguzeni na kuyaona mambo mnayotendewa nchini Misri!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 “Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli, uwaambie, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, alinitokea akaniambia: Nimewatazama, nami nimeona mliyotendewa huku Misri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli, uwaambie, ‘bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, alinitokea akaniambia: Nimewatazama, nami nimeona mliyofanyiwa katika Misri.

Tazama sura Nakili




Kutoka 3:16
31 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.


BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema.


Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii unayolala nitakupa wewe na uzao wako.


Akambariki Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Abrahamu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo,


Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.


Watu walitangaze jina la BWANA katika Sayuni, Na sifa zake katika Yerusalemu,


Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao, Wazingojeao fadhili zake.


Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?


Basi akatokea mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.


Musa akaichukua ile mifupa ya Yusufu pamoja naye; maana, alikuwa amewaapisha sana wana wa Israeli, akisema, Mungu hana budi atawajia ninyi; nanyi mtaichukua mfupa yangu kutoka hapa pamoja nanyi.


Makabila ya watu wamesikia, wanatetemeka, Wakazi wa Ufilisti uchungu umewashika.


BWANA akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe; na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende.


Yethro mkwewe Musa akamletea Mungu sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; na Haruni akaja, na wazee wote wa Israeli, wale chakula pamoja na mkwewe Musa mbele za Mungu.


Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.


Naye hakuweka mkono wake juu ya hao wakuu wa wana wa Israeli; nao wakamwona Mungu, wakala na kunywa.


Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea.


Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akafunika uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.


Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea.


Musa na Haruni wakaenda, wakawakusanya wazee wote wa watu wa Israeli.


Watu wakaamini, na waliposikia ya kuwa BWANA amewajia wana wa Israeli, na ya kuwa ameyaona mateso yao, wakainamisha vichwa vyao wakasujudu.


ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amekutokea.


Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;


Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.


watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiwa kwako.


Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.


Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.


Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa.


Muwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.


Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;


Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana akiwa katika nchi ya Moabu alipata habari kuwa BWANA alikuwa amewajia watu wake na kuwapa chakula.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo