Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia wako nitawatekea, hadi watakapokwisha kunywa.
1 Petro 4:9 - Swahili Revised Union Version Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung'unika; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Muwe na ukarimu nyinyi kwa nyinyi bila kunung'unika. Biblia Habari Njema - BHND Muwe na ukarimu nyinyi kwa nyinyi bila kunung'unika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Muwe na ukarimu nyinyi kwa nyinyi bila kunung'unika. Neno: Bibilia Takatifu Kuweni wakarimu kila mtu na mwenzake pasipo manung’uniko. Neno: Maandiko Matakatifu Kuweni wakarimu kila mtu na mwenzake pasipo manung’uniko. BIBLIA KISWAHILI Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung'unika; |
Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia wako nitawatekea, hadi watakapokwisha kunywa.
Gayo, mwenyeji wangu, na wa kanisa lote pia, awasalimu. Erasto, wakili wa mji, na Kwarto, ndugu yetu, wanawasalimu. [
Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.
Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkarimu, ajuaye kufundisha;
bali awe mkarimu, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake;
Lakini sikutaka kutenda neno lolote isipokuwa kwa ushauri wako, ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari.
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.