1 Petro 4:8 - Swahili Revised Union Version Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Zaidi ya yote pendaneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi. Biblia Habari Njema - BHND Zaidi ya yote pendaneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Zaidi ya yote pendaneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi. Neno: Bibilia Takatifu Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi. Neno: Maandiko Matakatifu Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi. BIBLIA KISWAHILI Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. |
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;
Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.
Lakini lengo la agizo hili ni kuleta upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.
Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali “ndiyo” yenu na iwe ndiyo, na “Hapana” yenu iwe hapana, msije mkaanguka katika hukumu.
jueni ya kuwa yeye amrejeshaye mwenye dhambi hadi akatoka katika njia ya upotevu, ataokoa roho ya mwenye dhambi kutoka mauti, na kufunika wingi wa dhambi.
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.