Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
Zekaria 14:1 - Swahili Revised Union Version Tazama, siku ya BWANA inakuja, ambayo mali mliyonyang'anywa itagawanywa kati yenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu. Biblia Habari Njema - BHND Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu. Neno: Bibilia Takatifu Siku ya Mwenyezi Mungu inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu. Neno: Maandiko Matakatifu Siku ya bwana inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu. BIBLIA KISWAHILI Tazama, siku ya BWANA inakuja, ambayo mali mliyonyang'anywa itagawanywa kati yenu. |
Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia;
Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo.
Umati mkubwa, umati mkubwa, wamo katika bonde la kukata kauli! Kwa maana siku ya BWANA i karibu, katika bonde la kukata kauli.
Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU; Kwa maana siku ya BWANA iko karibu; Kwa kuwa BWANA ametayarisha dhabihu, Amewatakasa wageni wake.
Yuda naye atafanya vita juu ya Yerusalemu; na huo utajiri wa mataifa wa pande zote utakusanywa, dhahabu, na fedha, na mavazi; vitu vingi sana.
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Angalieni, nitawatumia Eliya nabii, kabla siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya haijafika.
Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.
Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.