Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 14:1 - Swahili Revised Union Version

1 Tazama, siku ya BWANA inakuja, ambayo mali mliyonyang'anywa itagawanywa kati yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Siku ya Mwenyezi Mungu inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Siku ya bwana inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Tazama, siku ya BWANA inakuja, ambayo mali mliyonyang'anywa itagawanywa kati yenu.

Tazama sura Nakili




Zekaria 14:1
12 Marejeleo ya Msalaba  

Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.


Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.


Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.


Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia;


Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo.


Umati mkubwa, umati mkubwa, wamo katika bonde la kukata kauli! Kwa maana siku ya BWANA i karibu, katika bonde la kukata kauli.


Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU; Kwa maana siku ya BWANA iko karibu; Kwa kuwa BWANA ametayarisha dhabihu, Amewatakasa wageni wake.


Yuda naye atafanya vita juu ya Yerusalemu; na huo utajiri wa mataifa wa pande zote utakusanywa, dhahabu, na fedha, na mavazi; vitu vingi sana.


Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.


Angalieni, nitawatumia Eliya nabii, kabla siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya haijafika.


Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.


Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo