Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 14:14 - Swahili Revised Union Version

14 Yuda naye atafanya vita juu ya Yerusalemu; na huo utajiri wa mataifa wa pande zote utakusanywa, dhahabu, na fedha, na mavazi; vitu vingi sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Watu wa Yuda watapigana kuulinda mji wa Yerusalemu; utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka nchi ya Yuda utakusanywa: Watakusanya dhahabu, fedha na mavazi kwa wingi sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Watu wa Yuda watapigana kuulinda mji wa Yerusalemu; utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka nchi ya Yuda utakusanywa: Watakusanya dhahabu, fedha na mavazi kwa wingi sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Watu wa Yuda watapigana kuulinda mji wa Yerusalemu; utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka nchi ya Yuda utakusanywa: watakusanya dhahabu, fedha na mavazi kwa wingi sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na mavazi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo.

Tazama sura Nakili




Zekaria 14:14
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.


Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbayumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.


Tazama, siku ya BWANA inakuja, ambayo mali mliyonyang'anywa itagawanywa kati yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo