Kwani kuugua kwangu kwaja kana kwamba ni chakula, Na kunguruma kwangu kumemiminika kama maji.
Zaburi 102:9 - Swahili Revised Union Version Maana ninakula majivu kama chakula, Na kukichanganya kinywaji changu na machozi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Majivu yamekuwa chakula changu, machozi nayachanganya na kinywaji changu, Biblia Habari Njema - BHND Majivu yamekuwa chakula changu, machozi nayachanganya na kinywaji changu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Majivu yamekuwa chakula changu, machozi nayachanganya na kinywaji changu, Neno: Bibilia Takatifu Ninakula majivu kama chakula changu, nimechanganya kinywaji changu na machozi Neno: Maandiko Matakatifu Ninakula majivu kama chakula changu na nimechanganya kinywaji changu na machozi BIBLIA KISWAHILI Maana ninakula majivu kama chakula, Na kukichanganya kinywaji changu na machozi. |
Kwani kuugua kwangu kwaja kana kwamba ni chakula, Na kunguruma kwangu kumemiminika kama maji.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?
Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.