Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mika 7:17 - Swahili Revised Union Version

17 Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Watatambaa mavumbini kama nyoka; naam, kama viumbe watambaao. Watatoka katika ngome zao huku wanatetemeka na kujaa hofu. Watakugeukia wewe Mungu wetu kwa hofu, wataogopa kwa sababu yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Watatambaa mavumbini kama nyoka; naam, kama viumbe watambaao. Watatoka katika ngome zao huku wanatetemeka na kujaa hofu. Watakugeukia wewe Mungu wetu kwa hofu, wataogopa kwa sababu yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Watatambaa mavumbini kama nyoka; naam, kama viumbe watambaao. Watatoka katika ngome zao huku wanatetemeka na kujaa hofu. Watakugeukia wewe Mungu wetu kwa hofu, wataogopa kwa sababu yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Wataramba mavumbi kama nyoka, kama viumbe vinavyotambaa ardhini. Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka; watamgeukia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa hofu nao watakuogopa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Wataramba mavumbi kama nyoka, kama viumbe vitambaavyo juu ya ardhi. Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka; watamgeukia bwana Mwenyezi Mungu wetu kwa hofu nao watakuogopa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.

Tazama sura Nakili




Mika 7:17
27 Marejeleo ya Msalaba  

Wageni nao waliishiwa nguvu, Wakatoka katika ngome zao wakitetemeka.


Hofu ya BWANA ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda, wasipigane vita na Yehoshafati.


Wageni nao walitepetea, Walitoka katika ngome zao wakitetemeka.


Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.


Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi.


Uwatie hofu, ee BWANA, Watu wa mataifa na wajitambue kuwa wao ni binadamu tu!


Kwa hiyo watu walio hodari watakutukuza, Miji ya mataifa yatishayo itakuogopa.


Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.


Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.


Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha katika nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.


kama vile moto uchomapo vichaka, na moto uchemshapo maji; ili kuwajulisha adui zako jina lako, mataifa wakatetemeke mbele zako!


Mbwamwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema BWANA.


Nao watakuja na kutulia katika mabonde yaliyo ukiwa, na katika pango za majabali, na juu ya michongoma yote, na juu ya malisho yote.


Tazama, asema BWANA, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.


Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo, nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo.


Na atie kinywa chake mavumbini; Ikiwa yamkini liko tumaini.


Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na BWANA, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.


Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto, Na uharibifu mkali; Nitawapelekea meno ya wanyama wakali, Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini.


Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi huyo BWANA, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele zenu; kwa sababu hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno hili.


Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.


Basi, hao wote wawili wakajidhihirisha mbele ya ngome ya Wafilisti, na wale Wafilisti wakasema, Kumbe! Wale Waebrania wanatoka katika mashimo walimojificha!


Tufuate:

Matangazo


Matangazo