Zaburi 102:12 - Swahili Revised Union Version Bali Wewe, BWANA utaketi ukimiliki milele, Na jina lako litakumbukwa na vizazi vyote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, watawala milele; jina lako lakumbukwa vizazi vyote. Biblia Habari Njema - BHND Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, watawala milele; jina lako lakumbukwa vizazi vyote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, watawala milele; jina lako lakumbukwa vizazi vyote. Neno: Bibilia Takatifu Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, umeketi kwenye kiti chako cha enzi milele; sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wewe, Ee bwana, umeketi katika kiti chako cha enzi milele, sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote. BIBLIA KISWAHILI Bali Wewe, BWANA utaketi ukimiliki milele, Na jina lako litakumbukwa na vizazi vyote. |
Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.
BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.
Na kwa kuwa umeachwa na kuchukiwa, Hata ikawa hapana mtu aliyepita ndani yako, Nitakufanya kuwa fahari ya milele, Furaha ya vizazi vingi.
Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.